logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mourinho apewa marufuku ya mechi minne na shikisho la soka la Uturuki kwa semi za kibaguzi

Meneja wa Fenerbahçe, José Mourinho, amefungiwa michezo minne na kupigwa faini ya jumla ya £35,194

image
na Japheth Nyongesa

Football28 February 2025 - 13:08

Muhtasari


  • Hata hivyo Fenerbahçe ilitoa taarifa ikisema kuwa kauli za kocha huyo zilichukuliwa "vibaya kutoka katika muktadha wake".
  • Viongozi wa Fenerbahçe walithibitisha  kuwa klabu itakata rufaa dhidi ya adhabu zilizotolewa kwa mkufunzi Mourinho.

Meneja wa Fenerbahçe, José Mourinho, amefungiwa michezo minne na kupigwa faini ya jumla ya £35,194 kutokana na kauli alizozitoa za 'kibaguzi' baada ya debi ya Jiji la Istanbul dhidi ya Galatasaray.

Mourinho alituhumiwa na Galatasaray kwa kutoa kauli za kibaguzi baada ya mchezo huo wa siku ya Jumanne.

Hata hivyo Fenerbahçe ilitoa taarifa ikisema kuwa kauli za kocha huyo zilichukuliwa "vibaya kutoka katika muktadha wake".

Mechi hiyo ya sare ya 0-0 ilichezeshwa na mwamuzi kutoka Slovenia, Slavko Vincic, baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana na kuomba achezeshe mwamuzi wa kigeni.

Hata hivyo, mwamuzi wa nne alikuwa Mturuki na Mourinho alirudia tena kutoa lawama zake kuhusu waamuzi wa Kituruki wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mchezo.

Kocha huyo wa Kireno, mwenye umri wa miaka 62, alisema alikwenda katika chumba cha kubadilishia nguo cha waamuzi baada ya mchezo wa Jumatatu, akimwambia mwamuzi wa nne kwamba "kama ungekua mwamuzi, mchezo huu ungekuwa janga kabisa".

Alhamisi, Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) lilithibitisha kuwa litamchukulia hatua Mourinho kwa masuala mawili tofauti ya kinidhamu.

TFF ilisema itamwadhibu kwa "kauli zake za kudhalilisha na kuudhi kwa mwamuzi wa Kituruki" na kwa kauli za dhihaka na kuudhi kwa jamii ya soka ya Kituruki na waamuzi wa Kituruki".

Kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Chelsea, Manchester United, na Tottenham amepigwa marufuku ya kucheza michezo miwili kuwa uwanjani na amepigwa faini ya 117,000 lira za Kituruki (takriban £2,543).

Mourinho pia amepigwa marufuku ya michezo mingine miwili kwa "kitendo cha kutoupa heshima mchezo" wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mchezo na kupigwa faini nyingine ya £32,651.

Muafrika Didier Drogba, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea aliyewahi kufundishwa na mourinho, alimtetea kupitia mtandao wa kijamii kusema kocha huyo si mbaguzi.

Viongozi wa Fenerbahçe walithibitisha  kuwa klabu itakata rufaa dhidi ya adhabu zilizotolewa kwa mkufunzi Mourinho.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved